Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu.

Tukio hilo ni kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambapo amewasili leo Januari 11, 2017 na baadaye kufungua barabara ya Lamada – Bariadi yenye urefu wa kilomita 72.8 iliyojengwa na kampuni ya CCCC ya China.

Akiongea na wananchi mkoani humo katika kijiji cha Masanza, Busega amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inawatumika watanzania, hivyo amewaomba wananchi waiamini huku akisisitiza kauli yake ya kufanya kazi na kwamba hakutakuwepo chakula cha msaada, wananchi lazima walime mazao yanayostahimili ukame.

Pia, Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Busega kuwa tatizo la maji walilonalo Serikali italishughulikia na kuahidi kumtuma Waziri wa maji ili aweze kufika na kuangalia tatizo hilo.

Nape Nnauye afanya uteuzi
Vyuo 22 vyaitunishia misuli TCU

Comments

comments