Katibu wa Rais ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Ngusa Samike kwa niaba ya Rais Magufuli leo Agosti 24 2020, amewasilisha fedha za michango iliyotolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino Mkoani Dodoma.

Fedha hizo ziliwasilishwa kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya Suleiman Abdallah Matitu muda Mfupi baada ya swala ya Adhuhuri iliyofanyika katika msikiti uliopo hivi sasa.

Rais Magufuli amewapongeza na kushukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa msikiti mpya wa kisasa wilaya ya chamwino.

Amesema watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya Dini waliyonayo, hiyo ni udhibitisho wa umoja na mshikamano walionao Watanzania.

Aidha Rais Magufuli amesema msikiti huo utajengwa na jeshi la kujenga Taifa JKT na ujenzi unaanza wiki hii.

Agosti 23, 2020 Rais Magufuli alifanya harambee katika ibada ya uzinduzi Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Emmaculata. Katika harambee hiyo Rais alikusanya Zaidi ya shilingi millioni 48 na kutolewa kwa mifuko ya saruji na mchanga.

Mama ahukumiwa kwa kumkata nyeti mwanaye wa siku tatu
Lori la mafuta lawaka moto Morogoro.