Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd) chenye thamani ya shil. bilioni 200 mkoani Pwani na kuwataka watumishi wa umma kuacha urasimu wakati wa utoaji vibali kwa wawekezaji.

Ameyasema hayo mapema hii leo Kibaha Mkoani Pwani alipokuwa akizundua kiwanda hicho, ambapo amezikemea baadhi ya taasisi zinazoweka mazingira ya rushwa wakati wa utoaji vibali zikiwemo, NEMC, OSHA na Shirika la viwango TBS.

“Hili nilishaliona, ndio maana vibali vyote vya NEMC vimefutwa na kupitishwa na bunge la bajeti ya mwaka 2017/18 hii ilikuwa ni kwaajili ya kuvifanyia marekebisho na kuweka usawa katika utoaji vibali hivyo,”amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli katika hatua nyingine amezindua kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus na kiwanda cha Nondo cha Kiluwa hivyo amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwani Serikali iko nao bega kwa bega.

Audio: Diamond awaweka Wema Sepetu na Zari kwenye ngoma yake mpya ‘Fire’
Mgandilwa atoa siku tatu kulipwa deni la shil. 270 Kigamboni