Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameunga mkono mgomo wa wakulima wa korosho kwa kusema kuwa yuko pamoja nao bega kwa bega.

Maamuzi hayo ya Rais Magufuli yametangazwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwenye kikao na wakuu wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambacho kililenga kujadili juu ya hatua ya mgomo wa wakulima wa korosho juu ya kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka 2 iliyopita.

“Rais John Magufuli amewapongeza wakulima wa korosho kwa uamuzi wao wa kukataa kuuza kwa bei ndogo na kueleza yuko pamoja nao na kumtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, ajitathimini katika suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea.”amesema Majaliwa

Aidha, amesema kuwa hawaridhishwI na utendaji kazi wa bodi ya korosho ambao umekiuka maelekezo ya msingi ya Serikali katika kusimamia mfumo mzima wa zao la korosho uliopelekea kuvurugika kwa minada 2.

Wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara walilazimika kuingia kwenye mgomo wa kuuza zao hilo la Korosho kwa kile walichodai kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita huku gharama za uzalishaji zikiwa zimepanda.

 

Ijue faida ya bamia katika mwili na ngozi yako
Rais wa Uturuki aikomalia Saudi Arabia kutaja uliko mwili wa mwandishi aliyeuawa