Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewapasha waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera na kuwataka kila mmoja abebe msalaba wake.

Amesema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi(CCM), haitawajengea nyumba waathirika wa janga hilo, lililotokea Septemba 10, mwaka 2016.

Katika tetemeko hilo mamlaka za Serikali zilisema watu 17 walipoteza maisha, nyumba 2,o63 zilianguka, 14,081 zilikuwa kwenye hali mbaya baada ya kupata nyufa,na 9,471 zikipata nyufa kidogo.

“Haiwezekani Serikali ikajenga nyumba zote za wananchi wa Mkoa wa Kagera, haipo Serikali ya namna hiyo duniani. tunajua wanasiasa wengine watakuja kuwaambia Serikali itakuja kuwajengea majengo yenu, waambieni wawajengee wenyewe”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo,inakadiriwa kuwa tetemeko hilo lilikuwa ni kubwa kuliko yote yaliyotokea nchini, wananchi wapatao 126,315 wanauhitaji wa huduma za kibinadamu, kutokana na kuathirika na janga hilo.

 

Young Africans Wakomaa Na Point Za Mezani
Kocha Wa Ivory Coast Amnyima Raha Jose Mourinho