Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani  Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya maadhimisho ya kimataifa kuongeza  uelewa juu watu wenye ualbino yatakayofanyika juni 13 viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ualbino taifa (TAS),Nemes Temba ameeleza kwamba maadhimisho hayo kwa mwaka huu yatakuwa ya 11 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini  2006 na ya pili kimataifa tangu baraza la umoja wa mataifa kuitangaza rasmi juni 13 ya kila mwaka kuwa siku ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa ktika maadhimisho hayo wanatarajia kujumuisha kufanya huduma za afya ya saratani ya ngozi ambapo kwa tarehe 11 juni huduma hiyo itapatikana katika hospitali ya ocean road na tarehe 12 katika viwanja vya mnazi mmoja, pamoja na kufanya ziara ya bagamoyo na watoto waishio katika vituo mbalimbali Tanzania ambako wamepata hifadhi ya elimu na chakula kwa msaada wa UNISEF.

Hata hivyo akizungumzia suala la Serikali Bw.Temba amesema wanaipongeza serikali kwa kutambuauwepo wao katika jamii na  hata kama bajeti iliyoelekezwa upande wao ni ndogo lakini imewatambua na kupata mwakilishi katika serikali hii ya awamu ya tano.

Kwa upande wa Katibu Mkuu chama cha watu wenye Ualbino  Mussa Kabimba amesema kuwa kwa sasa hali ya ulinzi na usalama kwao  hairidhishi kwani mpaka sasa hakuna mpango mkakati uliowekwa na serikali kwa ajili ya kuwatia nguvuni wauaji kama kuhakikisha watu wenye ualbino wanaishi kwa amani katika nchi yao.

Ameongeza kuwa ni vyema serikali kwa sasa isaidie kwa kutenga fungu ambalo litasaidia watu wenye ualbino kupata matibabu na kliniki ya ngozi kama wasaidiwavyo wagonjwa wenye virusi vya ukimwi.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika tare 11 maka siku ya tar 13 huku kukiwa na maonyesho pamoja na burudani mbalimbali na kauli mbiu ya ikiwa ni ”haki ya ushiriki, haki ya ujumuishi , watoto wenye ulemavu wasikilizwe na walindwe

 

 

Audio: Simba imegonga mwamba kuinasa saini ya Kocha wa Zimbabwe
Lemonade yampaisha Beyonce, Avunja Rekodi Ya Wanamuziki Wote Wa Kike