Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya Mashujaa nchini ambapo kitaifa yanafanyika Mkoani Dodoma.

Hii inatajwa kuwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru 1961 kwa maadhimisho hayo kufanyika nje ya jiji la Dar es salaam huku pia ikiwa mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuwa Mgeni rasmi baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa taifa Octoba mwaka jana.

”Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu Mashujaa yatafanyika kitaifa mkoani Dodoma katika uwanja wa Mashujaa siku ya Jumatatu leo julai 25 asubuhi na kuanzia asubuhi na Mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli” Alisema Mkuu wa Mkoa Dodoma Jordani Rugimbana alipokuwa akiongea na wanahabari hapo jana.

Aidha katika siku ya maadhimisho matukio mbalimbali yatafanyika ikiwemo gwaride la maombolezo kutoka vikosi vya majeshi ya kujenga taifa na lile la wananchi pamoja shughuli za uwekaji wa taji la maua katika mnara silaha za asili bila kusahau upigaji wa mizinga.

Rugimbana amewataka wakazi kutoka sehemu mbalimbali za dodoma kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya mashujaa na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo, huku akitoa shukrani kwa Serikali kuupa heshima Mkoa huo ambao ni Makao Makuu ya nchi.

 

 

 

Ujerumani yapata Pigo lingine la usalama
Auawa na chui punde baada ya kutoka kwenye gari