Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkesha wa mwaka mpya  utakaofanyika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Askofu wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, Godfrey Malassy alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa kutakuwa na maombi  maalumu kwaajili ya kuliombea taifa.

“Kwa siku moja tutasali pamoja na wenzetu walio sehemu tofauti tofauti nchini, lengo kubwa ni kuliombea taifa na nchi yetu kwa ujumla ili izidi kuwa na amani.”amesema Malassy.

Aidha, amesema kuwa kutakuwa na maombi maalumu kwaajili ya Mkuu wa Nchi na viongozi wengine kwa kumaliza mwaka na kuingia mwaka mpya.

Mpango:Uchumi wetu unakua kwa kasi
UFC 207: Amanda Nunes 'amfunza adabu' Ronda Rousey