Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa ni lazima hata yeye ajitathmini kuhusu baadhi ya viongozi anaowachagua kwakua kuna baadhi wanakwamisha haki kutendeka kwa wananchi kutokana na kutofanyia kazi mambo ya msingi.

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria na kusema yeye ameumbwa kusema ukweli hivyo ataendelea kusema ukweli hata kama kuna watu unawaumiza.

“Watu wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania, ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo ndani ya Serikali lazima na mimi nijitathimini ninachaguagaje hawa watu ambao wanachelewesha chelewesha, hiyo ndiyo tathmini ambayo ninaanza kujifanyia kuanzia leo,”amesema JPM.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kinachomshangaza ni hatua nzuri ya serikali kupeleka ‘Legal Aid Act’ ya mwaka 2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini ‘regulation’ mpaka sasa hazijapelekwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo.

 

Video: Siri mpya za Lowassa zafichuka, Bunge laibua madudu kila kona
Walimu 'vicheche' wakalia kuti kavu