Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete leo Oktoba 23, 2018 amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Joseph pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mhe.Kikwete amesifia juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli na kumsihi aendelee kufanya kazi kwani kwa namna yeyote atamuunga mkono.

“Nimekuja kumsalimia nakumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yeyote kumpa nguvu tayari kumsaidia” Amesema Jakaya Kikwete.

Paco Alcacer: Sijutii kuondoka FC Barcelona
Anthony Martial kumalizana na Man Utd

Comments

comments