Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais John Magufuli amesema Kamati ya maadili na usalama na kamati Kuu ya CCM zilipitia majina yote zaidi ya 10,000 ya wana CCM walioomba kuteuliwa kugombea ubunge ili kuhakikisha hakuna atakayeonewa.

Amesema CCM ni chama kinachopendwa na hii ni kutokana na watu wa aina zote waliojitokeza kuomba nafasi mbalimbali na kufikia takribani elfu 43 ambapo amesema inawezekana chama hicho kimevyunja rekodi hata Afrika baada ya watu wengi kujitokeza kuomba nafasi za kugombea.

“Niwapongeze wajumbe wote wa NEC kwa kunipigia kura nyingi za NDIYO, mlikuwa wajumbe hamkuniangusha wajumbe, hata kwenye udhamini mmenipa wadhamini zaidi ya milioni 1.1. Nimedhaminiwa katika mikoa mingi sana ya Bara na Zanzibar”.amesema Rais Magufuli.

“Nawapongeza sana wana-CCM wote walioomba kuteuliwa kuwania nyadhifa mbalimbali, ubunge 10,367, uwakilishi 786, udiwani 33,094, hii inaonyesha CCM inapendwa sana, hakuna chama kingine ambacho watu wengi namna hii wamejitokeza, CCM ni chama kinachoheshimika”.

“Naomba niwahakikishie kuwa uchambuzi huu ulikuwa wa kina kwelikweli, tumetumia vyanzo vyetu vyote, nimepitia majina yote 10,367. Hatujampendelea mtu wala kumnyima mtu haki yake, tumewajadili wagombea wote kwa kina na kujiridhisha wenye sifa”. amesema Rais Magufuli.

Wa Nec 54 kikaangoni leo
Tonombe, Kisinda ndani ya Bongo