Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza mkoani Kagera ambapo wanatarajia kufanya mazungumzo ambayo yatafanyika mkoani humo.

Nkurunzinza amewasili mapema hii leo Mkoani Kagera na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli kisha kupigiwa mizinga 21 ya heshima na kukagua gwaride maalumu lililokuwa limeandaliwa kwaajili yake.

Aidha, mara baada ya ukaguzi wa gwaride hilo, viongozi hao wawili wanatarajiwa kuwa na mazungumzo maalumu ambayo mpaka sasa hayajajulikana yatalenga jambo gani ambalo limewakutanisha..

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli yuko Ziarani Kanda ya Ziwa na ambapo hapo jana alizindua barabara ya kiwango cha Lami ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Km 154 ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Video: Itazame ngoma mpya ya Aslay 'Baby'
Zitto kabwe apinga vikali matamko ya Tundu Lissu