Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5 hadi 7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi IKulu, jijini Dar es salaam, Humphrey Polepole na kumtuma awajulishe Watanzania na wana CCM kwamba wapuuze mijadala hiyo kwani jambo hilo halijawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama.

Hata hivyo, kupitia taarifa iliyotlewa na Ikulu, Rais Dkt. Magufuli amemuagiza Polepole kuwajulisha watanzania na wana CCM kuwa wasikubali kuyumbishwa au kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2017.

Joh Makini: Mimi na Fid Q, chochote kinaweza kutokea
Mgogoro wa shamba wasababisha vifo