Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa yeye yupo kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania hivyo hayuko tayari kuwaangusha.

Ameyasema hayo mapema hii leo mkoani Singida ambapo amewapongeza wawekezaji wanaojenga viwanda mkoani humo.

Amesema kuwa Tanzania ilipokuwa imefikia ni pabaya hivyo ni lazima kuvumiliana ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo.

“Mimi sitishwi na wala sitishiki, nipo kwa ajili ya Watanzania, kwa hiyo ninawatumikia Watanzania wote, hivyo nitaendelea na msimamo wangu wa kuwatumikia,” amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Dkt. Maguli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.

'Supermarkets' zasitisha kuuza nyama toka Afrika Kusini
Mwigulu aonya atakayeandamana ‘hata kuzunguka kitanda’