Rais JPM, ametangaza kufunga migodi endapo wawekezaji wa migodi ya madini wataendelea kuchelewa kufanya mazungumzo juu ya urejeshaji wa fedha walizozichukua.

Hayo yamezungumzwa katika eneo la  Kakonko Kigoma maghiribi mwa Tanzania, na kusema anawasubiri wawekezaji hao waje kwenye mazungumzo, lakini muda ukizidi, mazungumzo hayotokwepo na migodi itafungwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara akiwa kwenye ziara yake ya siku tatu. Amesema haiwezekani makampuni hayo yanaendelea kuwa kimya wakati wameshakubaliana kuanzisha mazungumzo haraka.

“Makampuni ya madini yaliyoahidi kukaa na serikali kuzungumza, wafanye haraka wakiendelea kuchelewa nitafunga migodi yote wanayomiliki” Rais John Pombe Magufuli.

Wakati huo huo, Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania imesimamisha shughuli za utoaji leseni za utafutaji na uchimbaji madini, mpaka tume ya madini itakapoundwa na kuanza kufanya kazi rasmi.

Barakah afunguka sababu za kuitosa Rockstar4000, awavaa 'mashabiki' hawa
Wawili wafariki baada ya daladala kugonga treni Dar