Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kutembea kifua mbele kwani nchi imepiga hatua kubwa katika maendeleo na kuzishangaza nchi nyingine.

Amesema Tanzania ni kati ya nchi tano barani Afrika ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Akihutubia umati uliofika kushuhudia kuwasili kwa ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli alisema kuwa watu wanashangaa kuona Serikali imenunua ndege bila mkopo.

“Uwezo wetu ni mkubwa mno na wa ajabu, tumeweza kufanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi. Watu wanashangaa Tanzania tumewezaje kununua ndege bila kukopa,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, alisema kuwa kuna watu ambao hawaridhiki kwa lolote wanalofanyiwa, hivyo aliwataka watanzania kuhakikisha wanalinda umoja na amani iliyopo.

Mahakama yaamuru Anudo Ocheng arejeshwe Tanzania
Polisi wamsaka Tumbili aliyeiba mtoto

Comments

comments