Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chile Juan Antonio Pizzi amewatoa hofu mashabiki wa mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye jana aliripotiwa kuwa majeruhi.

Pizzi amesema mshambuliaji huyo anakabiliwa na majeraha ya kiazi cha mguu na hatokaa nje kwa muda mrefu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Kocha huyo amesema Sanchez atakosa mchezo wa hii leo ambapo Chile watapambana na Colombia katika harakati za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, na huenda akamtumia kwenye mpambano ujao dhidi ya Uruguay.

“Tutamkosa Alexis Sanchez katika mchezo wa alkhamis dhidi ya Colombia, lakini niwatoe hofu mashabiki wake kwa kuwaambia kwamba mchezaji wao anajkabiliwa na majeraha, lakini sio kwa kiwango kikubwa kama ilivyoelezwa.”

Taarifa zilizoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari zilidai kuwa, Sanchez huenda akakaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma sita.

Kufuatia taarifa za kuumia kwa mshambuliaji huyo, baadhi ya mashabiki wa klabu ya Arsenal wameingia hofu ya kumkosa Sanchez katika mpambano wa ligi ya nchini England, ambapo Novemba 19 kikosi chao kitasafiri kuelekea Old Trafford kupambana na Man Utd.

Sergio Kun Aguero: Sina Ugomvi Na Pep Guardiola
MTV EMA Wakiri tuzo waliyompa Wizkid ni ya Ali Kiba, wampokonya