Mkataba wa kiungo wa klabu ya Manchester United, Juan Mata umebakiza miezi kumi na mbili kumalizika lakini mchezaji huyo ameonyesha nia ya kutaka kubaki Old Traffold baada ya kukataa mshahara wa pauni 375,000 kwa wiki kujiunga na ligi kuu ya China.

Pamoja na kutopewa kipaumbele na kocha Jose Mourinho katika kikosi cha kwanza Mata anaonekana kuridhika na maisha ya Mancheter na huenda akaongeza mkataba kuendelea kukipiga na kikosi cha Mourinho.

”Nina furaha hapa kuwa hapa, nimekuwa hapa kwa karibia miaka minne sasa baba yangu amefungua mgahawa wa kihispania na kwakuwa mabo ni mazuri ninafurahia kubaki hapa,” alisema Mata.

Kiungo huyo mshambuliaji alijiunga na Manchester United mwaka 2014 kwa kitita cha Pauni milioni 37.1 akitokea Chelsea.

Juan Mata has reportedly turned down a staggering offer to join the Chinese Super League

Bodi ya mikopo yatoa orodha ya watakaonufaika
Moze Iyobo kafanya makubwa kumbadilisha Aunty Ezekiel