Kikosi cha Atletico Madrid kimepata nguvu ya kuelekea kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya mahasimu wao wa mjini Madrid, Real Madrid, kufuatia taarifa za mshambuliaji wao Antoine Griezmann kuonyesha utayari wa kupambana.

Beki wa pembeni wa Atletico Madrid Juanfran, amefichua siri ya uwezekano wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Ufaransa kucheza mchezo huo muhimu, kutokana na kusisitiza alimuhakikishia suala hilo walipozungumza faragha.

Griezmann alipunguza matumaini ya kujumuika na kikosi cha Atletico Madrid mwishoni mwa juma hili, baada ya kupata jeraha mguu akiwa na timu yake ya taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Sweden.

Juanfran amesema mshambuliaji huyo ambaye ameshafunga mabao manane katika michezo kumi na nne aliyocheza tangu mwanzoni mwa msimu huu, anaendelea vizuri na ana matarajio makubwa ya kupambana na vijana na Zinedine Zidane.

Image result for Juanfran and GriezmannJuanfran akiwa na Antoine Griezmann

“Nilizungumza na Griezmann, na nilimuuliza kama kuna uwezekano wa kujumuika nasi katika mchezo dhidi ya Real Madrid? alinihakikishia yupo tayari kufanya hivyo,” Juanfran alizungumza wakati alipohojiwa na kituo cha radio cha Partidazo COPE.

Mchezo huo wa mahasimu wawili wa mjini Madrid, utachezwa kwenye uwanja wa Vincente Calderon siku ya jumamosi mishale ya saa nne usiku kwa saa Afrika mashariki.

Slaven Bilic: Tunajivunia Kuwa Na Payet
Wachezaji Wa Arsenal Wahofiwa Kuchoka