Raisi wa Heshima wa mchezo wa Judo Zanzibar mwenye asili ya Japani Abdul Halim Shimaoka alitoa ahadi kwa wazanzibar ya kufanya vizuri katika Mashindano ya kumi ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika tarehe 26-27 ya  mwezi huu wa Februari Mjini Bunjubura nchini Burundi.

Alisema wao kama Zanzibar wamejiandaa vizuri licha ya vikwazo mbali mbali walivyokumbana navyo ikiwemo mambo ya Siasa lakini anaamini vijana wake watarudi na ubingwa ambapo pia akijivunia wachezaji wake watatu waliopata mafunzo nchini Japani hivi karibuni.

“ Tulifanya maandalizi ya mwezi mzima kwa kujiandaa na mashindano haya, na vijana wangu wanaari sana na malengo yao ni  kufanikiwa kufika mbali katika mchezo huu wa Judo”.

Mbali na hayo Shimaoka alisema kitu chengine  anachojivunia ni wachezaji wake watatu waliopata Mafunzo ya Judo nchini Japani kuanzia mwezi Septemba hadi Disemba mwaka jana 2015, hivyo anaamini watarudi na kombe Zanzibar kutoka huko Burundi.

“ Najivunia wachezaji wangu watatu waliopata mafunzo kule Japani mwishoni mwa mwaka jana ambao ni Ali Juma, Hafidh Makame na Mbarouk Suleiman, hivyo vijana wangu watarudi na Ubingwa”. Alisema Shimaoka.

Nae mchezaji Salma Omar ambae anacheza mchezo huo kwa uzito wa kilo 52 ambapo pia ni mwanamke pekee mwaka huu kutoka Zanzibar kwenda katika Mashindano hayo huko Burundi.

Salma alimwambia muandishi wa Habari hii jinsi gani alivojiandaa katika mashindano hayo ambapo alisema ana ndoto za kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Jumuiya za Madola, hivyo lazima apigane ki kike ili aoneshe kama yeye ni mwanamke shujaa kutoka visiwani Zanzibar na anaajiamini atafanya vizuri.

“ Nina imani kwa vile nilovofanya mazoezi ntashinda tu, mana kimazoezi nipo sawa, nidhamu ninayo ya hali ya juu, walimu wananiamini , pia nimejifunza kutokana na makosa ya miaka ya nyuma, hivyo hakuna sababu ya kuwa nisifanye vizuri”.

“ Kuwa mwanamke pekeangu kutoka Zanzibar katika mashindano hayo si sabubu ya kufanya vibaya, ukweli ndo inanipa nguvu na kuzidi kujituma zaidi ili nirudi na ubingwa”. Alisema Salma.

katika mashindano hayo Zanzibar imepeleka wawakilishi wao watakaoshindana ambao wana uzito tofauti wakiwemo Azan Hussein na Ali Juma wao watashiriki Judo kwa Uzito wa kilo 60.

Abdul rabi Alawi na Mansabu Alawi ni ndugu hao watacheza Judo kwa wenye Uzito wa kilo 66.

Na kwa upande wa uzito wa kilo 73 yupo Hafidh Makame pekee ambapo kwa uzito wa kilo 81 atawakilisha Mbarouk Suleiman, wakati huo huo Rajab Kassim atashiriki kwa wenye uzito wa kilo 90 na Masoud Amour yeye atashiriki uzito wa kilo 100.

Mohd Abdul rahman na Iddi Othman watashindana uzito wa zaidi ya kilo 100.

Katika mashindano ya 10 ya JUDO ya Afrika Mashariki ambayo yatafanyika Burundi tarehe 26-27 ya mwezi huu wa pili ambapo mkuu wa msafara huo ni Yussuf Thabit akikamilisha idadi ya watu 17 wakiwemo wachezaji pamoja na viongozi.

Ligi Daraja la Pili (SDL) Kufikia Kikomo Mwishoni Mwa Juma
Sumaye amvutia Magufuli Upinzani