Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema kuwa iko haja ya kuwapo kwa sheria ya kuruhusu wanasiasa kuhama vyama bila kupoteza nafasi zao za uongozi katika vyama wanavyohamia.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda ambapo amesema kuwa jukwaa hilo limefikia hatua hiyo baada ya kuona itaokoa fedha za serikali katika kuendeleza nchi kihuduma za maendeleo.

“Kwa kuwa taifa linaingia katika kipinidi cha uchaguzi muda si mrefu ujao, Jukata tumetafakari na kuona ipo haja ya kuruhusu mfumo wa wanasiasa kuhama vyama pasipo kupoteza nafasi zao za kuchaguliwa,” amesema Mwakagenda.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kutokana na wimbi la wabunge na madiwani kuhama vyama kwa sababu mbalimbali na malalamiko ya Watanzania kuhusu gharama kubwa zinazotumika katika uchaguzi mdogo, ni bora ikatungwa sheria ya kuhama na vyeo vyao.

 

Mnyika: Bila Katiba Mpya uchaguzi hautakuwa huru na haki 2020
Ni kweli nina madeni kwani Chadema inawahusu nini- Kalanga