Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Mwadui FC, Jamhuri Kiweru maarufu kwa jina la Julio, amemtaka Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuachia ngazi mara baada ya kushindwa kuleta mabadiliko ya mpira nchini.

Ameyasema hayo mapema hii leo katika ofisi za shirikisho hilo alipokuwa amewasindikiza baadhi ya wacheza soka wa zamani akiwemo Ally Mayay ‘Tembele’ kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Rais wa Shirikisho hilo.

Julio amesema kuwa ni aibu kwa Shirikisho hilo na nchi kwa ujumla kuongozwa na watu wasiofahamu nini maana ya mpira hivyo amemtaka Malinzi kukaa pembeni ili kuwaachia wengine wanaoufahamu vizuri mpira.

“Ni aibu kubwa sana kwetu sisi Tanzania kuongozwa na watu ambao sio wa mpira, ukienda Ghana, Cameroon na nchi zingine zote, mashirikisho yao yanaongozwa na watu wa mpira, leo hii sisi tumeng’ang’ana na watu ambao hawana uelewa na mpira, namshauri Malinzi aachie ngazi,”amesema Juilio.

 

Azarenka kupambana na Risa Ozaki
Gianluigi Donnarumma Arushiwa Fedha Bandia

Comments

comments