Kocha wa zamani wa klabu za Mwadui FC na Simba SC Jamuhuri Kihwelo “Julio” ameibuka na kuponda ligi ya Tanzania bara kwa kusema katika ligi zote Afrika mashariki na kati ligi hiyo ndio ligi mbovu kuliko zote.

Julio ameiponda ligi kuu ya Tanzania bara kwa kutumia kigezo cha uwezo wa mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel okwi, ambaye amewahi kuzitumikia Simba SC na Young Africans kwa nyakayti tofauti.

Kocha huyo amesema kiwango cha okwi ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Al Ittihad inayoshiriki ligi kuu ya Misri, kimeporoka lakini alipokua Tanzania alionekana kuwa bora, kutokana na udhaifu wa ligi aliyokua anacheza.

Amesema ni dhahir kiwango cha mshambuliaji huyo kutoka nchini Uganda, kimetoa taswira ya udhaifu wa ligi ya Tanzania bara ambayo kila kukicha imekua ikisifiwa kuwa bora katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

“Mimi naomba niwaulize hivi yule Okwi si mzee lakini si anacheza mpira, lakini anaoneka mzuri akija hapa kwetu huko nje hafanyi lolote,”

“Si yule Yuko Nchini Misri anafanya nini kule, lakini hapa anaonekana mkali kwa sababu wachezaji hawajitumi. Mfano anakutana na timu kama Ndanda, wachezaji wana njaa hawajalipwa baadhi ya mishahara yao unadhani hali itakuaje si watawafunga tu.” Alisema Julio.

Okwi alijiunga na Al Ittihad mwaka 2019, na tayari ameshaitumikia klabu hiyo katika michezo 13 na kufunga mabao mawili.

Ndugulile akanusha taarifa ya kuumwa
Songea: hofu yatanda, ardhi iliyotitia