Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Nape Nnauye, kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wadau wa michezo wameendelea kumpongeza Nnauye kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.

Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kocha wa Mwadui FC ambaye timu yake itashuka uwanjani Desemba 19 kuikabili Ndanda FC, amesema amefurahishwa na uteuzi huo huku akisema sekta ya michezo imepata Waziri kijana.

Julio, amedai kuwa unaupongeza uamuzi wa Rais Magufuli kumteua Nape kuwa Waziri atakaeshughulikia michezo kwani alichofanya ni sahihi.

Katika hatua nyingine, Gulio amedai kusikitishwa na taarifa zilizochapishwa kwenye baadhi ya magazeti kuwa amemuomba Waziri huyo kuanza na TFF kwa kuwa ina uozo mwingi.

Amedai kuwa habari hizo hazina ukweli kwa kuwa haijawahi kusema hivyo. Aliongeza kuwa hakutaka mtu amsemee kwani ana akili timamu na anapotaka kusema linalomhusu yeye, “hakuna mtanzania asiyemjua kuwa mimi ni muwazi na naweza kusema dakika yoyote. ”

Amesisitiza kuwa anakumbuka kuna mwandishi alimuuliza kuhusu Nape, na kudai kuwa mwandishi huyo aliandika habari ya upotishaji yenye lengo la kumgombanisha na Nape. Alisema waandishi wenye tabia hiyo atawapeleka mahakamani haraka.

Jumamosi ya Desemba 12, Julio, alikiongoza kikosi cha Mwadui kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja Stand United na kukisaidia kikosi chake kufikisha pointi 18 kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara.

Utafiti: Uongozi wa Nchi Hupunguza Umri wa Kuishi, Hatari kwa Afya
Hans Pope Atoa Ahadi Nzito Kwa Wanasimba