Aliyewahi kuwa Kocha wa Simba SC kwa nyakati tofauti Jamuhuri Kiwelu ‘JULIO’ ana wasiwasi huenda klabu hiyo ikaendeleza ufalme wa mataji kwa muda mrefu.

Julio ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa Simba SC, ameonesha wasiwasi baada ya kikosi cha Msimbazi kuifunga KMC FC mabao 2-0, jana Jumatano usiku.

Julio amesema kuna haja kwa timu nyingine kujipanga vizuri kama ilivyo Simba SC, ili kubadilisha ladha ya soka la ushindani na kuwapokonya Kombe la Ubingwa wababe hao.

“Kama timu nyingine hazitojipanga kama Simba walivyojipanga basi Simba itabeba ubingwa kila siku mpaka mpira wenyewe hautakuwa na ladha,” amesema kocha Julio baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya KMC FC.

Ushindi dhidi ya KMC FC unaifanya Simba SC kufikisha alama 76 ambazo zinaweza kufikiwa na Young Africans pekee, endapo itashinda michezo yake miwili iliosalia.

Sababu za Tasisi za kidini kutolipa kodi
Ndoto za ubingwa Young Africans bado zipo