Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Iimemrudisha, Jamhuri Kihwelu kugombea nafasi ya ujumbe ya uwakilishi wa mkoa wa Dar es salaam huku wenzie wanne ikiwakata kwa kosa la kufanya Kampeni kabla ya muda.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF  Wakili, Revocatus Kuuli amesema kuwa Julio amerudishwa mara baada ya kamati kupata uthibitisho wa elimu yake kitu ambacho kilikuwa kigezo kikubwa.

“Kamati iliomba uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani (NECTA) ambalo lilirudisha majibu kuwa Julio ana elimu ya kidato cha nne, kitu ambacho kilikuwa kigezo kikubwa cha kugombea nafasi hiyo,”amesema Kuuli

Aidha, kamati hiyo pia imewaengua wagombea wanne wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji baada ya kujiridhisha kuwa walifanya kampeni kabla ya muda wake hivyo kupoteza sifa ya kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo, wagombea walioenguliwa na nafasi zao ni pamoja na Shafih Dauda (Dar es salaam), Benista Lugola (Shinyanga, Simiyu), Ephraim Majinge (Mwanza, Mara), na Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa)

Jiji la Mwanza lapongezwa kwa utunzaji mazingira
Video: CUF washangazwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Prof. Lipumba