Wakati tume ya uchaguzi ya Taifa (NEC) ikiendelea kutangaza matokeo ya urais, mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji amewasilisha pingamizi rasmi na kuiondoa Chadema katika zoezi la utangazaji wa matokeo ya urais yanayoendelea.
Awali, Duni alifika katika eneo la ukumbi wa Julius Nyerere wakati zoezi likiendelea akidai kuwa amefika kuwasilisha hati ya pingamizi ya matokeo lakini walinzi walimzuia.
Hata hivyo, Duni alifuata maelekezo ya walinzi hao na kuwasilisha pingamizi na kuondoa ushiriki wa Chadema katika matangazo ya matokeo yanayoendelea.
Barua rasmi ya PETITION na kuondoa participation ya CHADEMA katika utangazwaji wa matokeo tume na kuondoa uwakilishi pic.twitter.com/RcxCC6v2sQ
— Shilinde! (@Erickshilinde) October 29, 2015
Chadema na vyama vinahyvounda Ukawa walipinga utaratibu wa utangazaji matokeo unaoendelea kwa madai kuwa kura zinazotangazwa haziendani na kura zilipatikana katika baadhi ya vituo hivyo zoezi hilo limelenga katika kumpendelea mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).