Baada ya safari ya zaidi ya miaka mitatu ya masomo nchini China, hatimaye mkali wa RnB, Juma Jux amehitimu masomo yake.

Kupitia Instagram, Jux ametoa taarifa ya kuhitimu masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT/IT) aliyoyasotea nchini humo.

“Mama I made It,” ameandika Jux kwenye moja kati ya picha alizoweka zikionesha amehitimu masomo ya elimu ya juu.https://dar24.com/audio-diamond-awaweka-wema-sepetu-na-zari-kwenye-ngoma-yake-mpya-fire/

Watu wengi wamempongeza kwa kufanya vyema kwenye elimu na muziki, akiwemo rapa Nikki wa Pili.

“Eeeh hongera kwa kuamsha dude baba @juma_jux tunakubaliana kuwa shule na muzik havitengani…..hope madogo kona zote tz wamelipata somo,” ameandika Nikki wa pili.

Katika hatua nyingine, mpenzi wake, Vannessa Mdee amewakejeli waliokuwa wakidai picha za uthibitisho kama anasoma kweli nchini China, katika ujumbe wake wa kumpongeza.

“Congratulations @juma_jux U finally done ✅ and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE,” ameandika Vee Money.

Dar24 inampongeza Jux kwa hatua aliyoipiga. Ni muziki na Shule.

Mohamed Salah Awasili Liverpool
Weusi wasaka saini 5000 waachie ‘Naliamsha Dude’ kama Gwajima