Mlinda mlango wa klabu ya Kagera Sugar, Juma kaseja ameiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa bao1-0 dhidi ya Simba katika mchezo uliopigwa leo uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo ulioudhuriwa na na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Simba wamefungwa kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi ya Vodacom Tanzania bara huku Juma Kaseja akidaka penati iliyopigwa na Okwi dakiaka ya 90.

Simba walikuwa hawajapoteza mchezo wowote na leo wangeweza kuweka rekodi ya kipekee ya kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo jambo ambalo limeshindikana baada ya kupoteza mchezo wa leo.

Simba wamekabidhiwa ubingwa rasmi leo wakiwa wamevuna jumla ya pointi 68 katika michezo 29 walioshuka dimbani mpaka sasa.

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 20, 2018
West Ham yamnyemelea Manuel Pellegrini