Matokeo mabovu yanayoziandama timu za mkoa wa Tanga yamezidi kuwaweka njia panda wadau wa soka huku wakiwa hawana matumaini ya kuona ligi kuu ya Tanzania hapo mwakani msimu ujao.

Timu 3 za Tanga, African Sports, Coastal Union na Mgambo JKT zipo katika nafasi 3 za mwisho katika eneo la kushuka daraja.

Matokeo hayo yamepelekea kujiuzulu kwa viongozi ndani ya wana ‘kimanumanu’ African Sports huku vingozi hao waliojiuzulu wakisema kukosekana kwa umoja na ushirikiano ndiyo chanzo cha wao kujiweka pembeni, wakati kwa upande wa Coastal Union shinikizo la muda mrefu kutoka kwa wanachama liliwafanya katibu mkuu Kassim El Siagi na meneja wa timu Akida Machai kujiuzulu nafasi zao.

Wadau wa soka mkoa wa Tanga wanasema kujiuzulu kwa viongozi hao ni kukwepa lawama kwani ni muda mrefu walitakiwa kufanya hivyo lakini walikuwa wakaidi.

Leo hii mwakilishi wa vilabu Juma Mgunda amejitokeza na kusema utawala ‘bomu’ wa vilabu hivyo ndiyo sababu kubwa ya kufanya kwao vibaya na pia suala la ubaguzi miongoni mwa wanachama na viongozi nalo ni tatizo jingine linalosumbua vilabu vya jijini Tanga.

Mgunda amesema viongozi hao walifanya kosa kubwa la kuwagawa watu ili waweze kuwatawala lakini kitu muhimu ni kuwa kila mwana Tanga aseme ukweli wa suala hilo.

Wadhamini Wa UEFA Champions League Kukarabati Viwanja Dar
Purukushani Za Man Utd Kumpa Ulaji Mauricio Pochettino