Kocha Mkuu wa Muda wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda mapema leo Ijumaa (Septemba 23) majiara ya Asubuhi alitembelea mazoezi ya kikosi cha Coastal Union yanayoendelea Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Mgunda alirejea jijini Tanga kwa mapumziko mafupi, kufuatia kusimama kwa Ligi Kuu Tanzania kupisha michezo ya Kimataifa ya Kalenda ya FIFA.

Kocha huyo Mzawa aliyeiongoza Simba SC katika michezo mitatu pasi na kuruhusu nyavu za kikosi chake kutikiswa, alifika Uwanja wa Mkwakwani na kuzungumza na Benchi la Ufundi ambalo kwa sasa linaongozwa na Kocha kutoka Kenya Yusuph Chipo kisha alikutana na wachezaji na baadae wakapiga picha ya pamoja.

Amewatakia kheri Wachezaji na Benchi la Ufundi la Coastal Unioni katika Uwanja wa Mkwakwani kwenye mapambano yao Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Hata hivyo Kocha huyo anatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam wakati wowote, ili kuendelea na kazi ya kukiandaa kikosi cha Simba SC kilichofunga safari kuelekea Kisiwani Unguja (Zanzibar), kwa ajili ya Michezo ya Kirafiki dhidi ya Kipanga FC na Malindi FC.

Mgunda alijiunga na Simba SC akitokea Coastal Union, siku chache kabla ya kucheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya mabingwa barani Afrika Hatua ya awali dhidi ya Mabingwa wa Malawi Nyasa Big Bullet, akichukua nafasi ya Kocha Zoran Maki aliyefikia makubaliano na kuvunjwa kwa mkataba wake na Uongozi wa Msimbazi mwishoni mwa mwezi Agosti.

Juma Mgunda amekua na historia kubwa na klabu ya Coastal Union akiitumikia kama mchezaji kwa muda mrefi na baadae kuwa Kocha Mkuu kwa vipindi tofauti.

Uviko-19 yarudisha nyuma vita ya UKIMWI, Malaria
Wananchi walalamikia 'Popobawa' DC asema wasimsingizie