Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema Mipango na mikakati ya kuhakikisha wanaikabili vyema Coastal Union imeanza rasmi jijini Dar es salaam, baada ya kuwasili wakitokea Mkoani Kilimanjaro jana Jumatatu (Novemba 28).

Jumapili (Novemba 27) Simba SC ilicheza ugenini dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa Ushirika-Moshi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, yaliwekwa kimianina Washambuliaji Moses Phiri aliyefunga mawili na John Bocco.

Kocha Mgunda amesema tayari ameshaanza mipango ya kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, ambapo anaamini mchezo huo utakua mgumu, kutokana na ubora wa wapinznai wao.

Amesema ameanza kukiandaa kikosi chake ili kufanikisha lengo linalokusudiwa na Benchi lake la Ufundi pamoja na Mashabiki wa Simba SC, ambao siku zote wamekua wakihitaji kuona timu yao inapata ushindi.

“Baada ya kumaliza mchezo wetu na Polisi Tanzania, nilipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wangu, kubwa nililowaambia tunakwenda kucheza na Coastal Union na kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha tunaendeleza mazuri kupitia mchezo huo.”

“Ninajua utakua mcheza mzuri kwa sababu Coastal Union wana kikosi kizuri ambacho kina uwezo wa kushinda, kwa hiyo tutajipanga zaidi katika Uwanja wa Mazoezi ili tuweze kwenda Tanga kupata matokeo mazuri.”

“Mimi kuwa nyumbani Tanga sio sababu rahisi kwa sisi kwenda Mkwakwani kupata ushindi, kikubwa hapa ni kujiandaa ili kuweza kukabiliana na wenzetu wa Coastal Union.” amesema Juma mgunda

Kocha huyo Mzawa atakua anarejea Uwanja wa Mkwakwani kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka mwezi Septemba 2022 kwa ajili ya kujiunga na Simba SC iliyomchukua kama Kaimu Kocha Mkuu.

Mshambualiji Coastal Union awaangukia wadau
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 29, 2022