Mlinzi wa timu ya Kagera Sugar Juma Said Nyosso anatarajiwa kupandishwa Mahakamani, kutokana na kutenda kosa la jinai wakati akitoka nje ya uwanja.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, RPC Agustine Ollom na kusema bado wanamshikilia mchezaji huyo wa Kagera na endapo watakapomaliza mahojiano naye wanatarajia kumpeleka Mahamakani kwa ajili ya mashtaka yake.

“Bado mtuhumiwa yuko mahabusu anaendelea kuhojiwa na yule majeruhi yupo hospitali kwa hiyo tunategemea madaktari wakatakavyo kuwa wamepita hii ’round’ ya asubuhi watatupa hali yake jinsi anavyoendelea. Juma Nyoso amefanya kosa la jinai hivyo sisi tutampeleka Mahakamani mapema itakavyowezekana na huko ndipo itakapojulikana kama alitenda kosa au laa na mwisho kutolewa adhabu juu yake”, alisema RPC Agustine Ollom.

Juma Said Nyosso alikamatwa jioni ya jana (Jumatatu) baada ya mechi kumalizika dhidi ya Simba katika dimba la Kaitaba ambapo wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanaelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa bahati mbaya mmoja ya mashabiki inasemekana alimpulizia vuvu zela Nyosso ndipo naye alipompiga shabiki huyo mpaka kupoteza fahamu.

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram amesema kuwa lau angekosa uvumilivu basi angekuwa tayari amegombana na mchezaji wa klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso hapo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao kufuatia mchezaji huyo kumsukuma pasipo sababu.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 24, 2018
Ushahidi wa sauti wazua taflani kesi ya Sugu