Serikali ya Rwanda, imeishutumu Jumuiya ya kimataifa kwa kuchochea mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, baada ya Marekani kuishinikiza Rwanda kusitisha uungaji mkono kwa waasi katika eneo hilo.

Vincent Biruta jana jioni alitowa taarifa akisema mwelekeo usiofaa na unaopotosha unaoonyeshwa na jumuiya ya Kimataifa unaendelea kuongeza tatizo, uingiliaji kutoka nchi za nje na matamshi ya kuamrisha ni mambo yanayohujumu jitihada za kikanda za usuluhishi.

Waandamanaji wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe unaokataa vita nchini DRC. Picha ya AP

Juhudi za kutafuta amani zinazowahusisha maafisa wa jumuiya ya Afrika Mashariki na makundi mbali mbali ya waasi wa Kongo zinaendelea huko Nairobi Kenya na Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda pia anasema wasiwasi wa nchi yake unapaswa kushughulikiwa.

Serikali ya Rwanda, mara kadhaa imekuwa ikiilaumu Serikali ya Kongo kuhusu mgogoro wa mashariki mwa nchi yake, na kuishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kufumbia macho suala la DRC kuwaunga mkono waasi wa FDLR.

Young Africans kushusha chuma cha Afrika
Fei Toto awaahidi mazito mashabiki Young Africans