Baada ya miongo sita iliyopita (tangu 1963), Sayari kubwa zaidi katika mfumo wa jua, Jupiter iliyo umbali wa takriban maili milioni 600 kutoka uso wa Dunia, itaikaribia zaidi Dunia.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA), limesema mtazamo wa uso wa Dunia, upinzani hutokea ambapo kitu cha unajimu kinapoinuka mashariki wakati Jua linatua magharibi, na kuweka uvuli wa Jua pande tofauti za Dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter NASA imesema, “Stargazers: Jupiter itakaribia Dunia baada ya miaka 59! tarajia kuona kwa ubora zaidi Septemba 26. Darubini inatosha kukupatia maelezo fulani, utahitaji kuwa na darubini kubwa ili kuona alama ndogo nyekundu.”

Jupiter, sayari kubwa zaidi katika mfumo wa jua, itakaribia zaidi Dunia tangu mwaka 1963. (Picha na Nation World News)

Jupiter, huonekana kwa ukubwa na kung’aa kila baada ya miezi 13 kuliko wakati wowote wa mwaka, na hatua ukaribiaji wa uso wa Duniahutokea kwa sababu Dunia na Jupiter hazizunguki Jua katika duara kamili, kutokana na kupita kwa umbali tofauti kwa mwaka mzima.

Njia ya karibu zaidi ya Dunia hufanana na upinzani mara chache, na kwa mwaka huu kutakuwa na mshangazo kwani njia yake ya karibu, itakuwa takriban maili milioni 367 kutoka uso wa Dunia, umbali sawa na ilivyokuwa kwa mwaka 1963.

Mtafiti wa astrofizikia katika Kituo cha Ndege cha Marshall Space huko Huntsville – Alabama, Adam Kobelski alisema bendi na tatu au nne za satelaiti za Galilaya (miezi), zitaweza kuonekana kwa darubini yenye viwango.

Kupitia chapisho la NASA, Kobelski alisema, “Ni muhimu kukumbuka kuwa Galileo aliona miezi hii na macho ya karne ya 17, mojawapo ya hitaji kuu litakuwa uwekaji thabiti kwa mfumo wowote utakaotumia.”

Hata hivyo, Mtafiti huyo anapendekeza utumiaji wa darubini kubwa yenye ukubwa wa inchi 4 au zaidi, ili kuona eneo jekundu la Jupiter kwa undani na baadhi ya vichujio katika safu ya kijani na samawati vitaboresha mwonekano wa vipengele hivyo.

“Maoni yanapaswa kuwa mazuri kwa siku chache kabla na baada ya Septemba 26, kwa hiyo, tumia fursa ya hali ya hewa nzuri kwa kila upande wa tarehe hii ili kutazama pembeni ya Mwezi, usio angavu zaidi angani usiku,” alifafanua Kolbelski.

Cedric Kaze: Tuna uwezo wa kushinda popote
Hersi Said kumaliza tofauti Young Africans