Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann ameripotiwa kuiweka sokoni nyumba anayoishi mjini California kwa kiasi cha dola million 1.7.

Kocha huyo kutoka nchini Ujerumani, ameripotiwa kufanya hivyo kwa kuhusishwa na mipango ya kutaka kutimuliwa kazi, kufuatia kikosi cha Marekani kupata matokeo mabaya katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Klinsmann mwenye umri wa miaka 51, alianza kukinoa kikosi cha Marekani mwaka 2011 na alikiongoza katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil.

Kupoteza mchezo dhidi ya Guatemala uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kwa kukubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri, na kulazimnishwa matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Trinidad na Tobago, kumeonyesha kuwagusa viongozi wa shirikisho la soka nchini Marekani hadi kufikia hatua ya kuanza kumjadili kocha huyo.

Suala kubwa linalowafanya viongozi wa shirikisho la soka nchini humo kuhoji kipigo hicho, ni kuhusu uwezo wa Klinsmann ambao unahisiwa huenda ukawa umefikia kikomo kutokana na mwenendo wake kutoridhisha.

Jumba la kifahari la kocha huyo ambalo limewekwa sokoni, linakadiriwa kuwa na eneo la mita za mraba 3,000, ambalo kwa nje limetawaliwa na bustani za kuvutia.

Huenda hatua ya kuiweka sokoni nyumba hiyo, ikawa imemshutua kocha huyo kwa kuamini mkataba wake utakatishwa wakati wowote kuanza sasa, hivyo anaamini ni wakati mzuri kurejea nyumbani kwao Ujerumani ili akasake mahala pengine pa kufanya kazi.

Klinsmann alipewa jukumu la kuhakikisha kikosi cha timu ya taifa ya Marekani, kinafanikiwa kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.

Katika harakati hizo Marekani imepangwa katika kundi la tatu katika michezo ya kufuzu kupitia ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF) sambamba na timu za Saint Vincent na the Grenadines, Guatemala pamoja na Trinidad na Tobago.

Katika mismamo wa kundi hilo Marekani inakamata tatu ya tatu kwa kufikisha point 4, nyuma ya Guatemala wenye point 6 huku Trinidad na Tobago wakiongoza kwa kumiliki point saba na  Vincent na the Grenadines wanaburuza mkia kwa kutokua na point.

Marekani imepoteza mchezo mmoja, kushinda mmoja na kutoka sare mmoja.

Dogo Janja aipiga teke shule
Rais Wa Uganda Athibitisha Kuguswa Na Msiba