Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema hana budi kuelekeza nguvu zake katika nafasi nne za juu, baada ya kushindwa kufikia lengo la kuingia kwenye mbio za ubingwa kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Klopp amezungumza na vyombo vya habari na kukiri jambo hilo, ambapo amesema kuna haja ya kuanza kujielekea katika mfumo wa kusaka namna ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.

“Nitaridhika sana endapo nitaiwezesha Liverpool kumaliza nafasi nne za juu, lengo langu kubwa tangu mwanzoni mw amsimu huu lilikua hapa, japo tulionekana kuwa na nia ya kuufukuzia ubingwa wakati fulani, lakini kwa sasa mambo yamekwenda ndivyo sivyo.

“Inanilazimu kurudi katika lengo langu na nitahakikisha kila hatua tunayoipiga katika michezo iliyosalia tunafanikisha ushindi ili kusalia katika lengo letu. Najua lengo hili litakua ni furaha kwa kila mmoja wetu, kwa sababu tutakua tumeingia kwenye mpango mwingine wa kupambana barani Ulaya.” Amesema Klopp.

Klopp amezungumzi jambo hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliokua na lengo la kuelezea maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo Liverpool watakua wageni wa West Bromwich Albion siku ya jumapili katika mchezo wa ligi ya England.

Katika mchezo huo Liverpool watawakosa viungo Adam Lallana na Jordan Henderson, ambao bado ni majeruhi.

Serikali yamkalia kooni mkandarasi, yataka amalize ujenzi kwa wakati
Mabilioni Yaliyofichwa Kwenye Jumba la Mwanasiasa Yanaswa