Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp huenda akaizidi keta klabu ya Man Utd katika mpango wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Senegal pamoja na klabu ya Southampton, Sadio Mane.

Klopp ameonyesha dhamira hiyo, kufuatia kuafiki mpango wa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambao huenda ukamgharimu kiasi cha Pauni milioni 25.

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, ameonyesha kuwa na dhamira ya kweli katika mpango huo, tofauti na ilivyo kwa Man Utd ambao mara kadhaa hawajihusishi sana na harakati za usajili wa Mane.

Endapo Mane, ataondoka Southampton, wakati wa majira ya kiangazi kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 25, ataiwezesha klabu hiyo kujipatia faida ya Pauni milioni 13.

Miaka miwiwli iliyopita, The Saint walimsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 12, akitokea nchini Uswiz alipokua akiitumikia klabu ya Salzburg.

Klopp alianza kuvutiwa na Mane, tangu alipoonyesha kiwango cha hali ya juu wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England msimu uliopita, kati ya Southampton dhidi ya Liverpool, ambao ulimalizika kwa majogoo wa jiji kukubali kisago cha mabao matatu kwa mawili.

Sitaki Nataka Za Slaven Bilic Kwa Alexandre Lacazette
James Rodriguez Aanza Msako Wa Nyumba Mjini Manchester