Mabingwa wa soka nchini England Chelsea FC, wameonyesha kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili beki kutoka Uholanzi na klabu ya Southampton Virgil van Dijk.

Gazeti la The Sun limeandika kuwa, Chelsea wapo mstari wa mbele katika dili hilo na kuwaacha Liverpool ambao walikua wa kwanza kuonyesha nia ya kumsajili beki huyo.

Meneja wa majogoo wa jiji Jurgen Klopp ameonyesha kukata tamaa na mpango wa kumsajili beki huyo, hali ambayo inasemekana kutoa mwanya kwa The Blues kupewa nafasi ya kufanikisha dili hilo.

Kwa sasa Van Dijk anafanya mazoezi ya pekee yake, huku uongozi wa Southampton ukitangaza kiasi cha Pauni milioni 50 kama ada yake ya uhamisho.

Hata hivyo Chelsea wanaelezwa kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa, ili kufanikisha mpango wa kumnasa Van Dijk.

Kaburu, Aveva Warudishwa Rumande
Wabunge 2 Chadema watiwa mbaroni