Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool, Jurgen Klopp amesema bado kuna nafasi ya kuimarika kama kikosi chake kinataka kupigania taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.

Liverpool ambao mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa ligi ilikuwa mwaka 1990, waliicharaza Hull City kwa mabao 5-1 mwishoni mwa juma lililopita na kupaa hadi mpaka katika nafasi nne kwenye msimamo wa ligi, wakiwa nyuma ya vinara ManCity kwa tofauti ya point tano.

Liverpool wameshinda michezo migumu ya ugenini dhidi ya Arsenal na Chelsea huku wakiwababua mabingwa Leicester City kwa mabao 4-1 msimu huu.

Mechi pekee waliyopoteza ni ile waliyofungwa na Burnley mabao mawili kwa sifuri.

Akihojiwa, Klopp amesema ni kweli kwa sasa wanacheza vizuri lakini bado kuna nafasi ya kuimarika ili waweze kuendeleza wimbi lao la ushindi.

Yaya Toure Awahurumia Wabaguzi Wa Rangi
Mambo 3 yanayofelisha maisha