Meneja wa majogoo wa jiji (Liverpool) Jurgen Klopp amepangua taarifa za kutaka kuondoka kwa mshambuliaji wake kutoka nchini England Daniel Sturridge, ambaye anadaiwa kukasirishwa na kitendo cha kuweka benchi wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tottenham.

Klopp amesema taarifa za Sturridge kutaka kuondoka Anfield hazimuingii akilini na haamini kama mshambuliaji huyo alikua chanzo cha habari hizo ambazo zilisambaa mara baada ya mchezo wao dhidi ya Spurs ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani ambaye alikinoa kikosi cha Borussia Dortmund kwa mafanikio makubwa, amesisitiza kuendelea kuwa na mshambuliaji huyo, na hadhani kama kuna tofauti baina yao zaidi ya vyombo vya habari kuanza kuleta uchokonozi.

“Daniel Sturridge ni mshambuliaji wa kiwango ambacho kinakihitaji katika kikosi changu na ninatarajia kumtumia mara kwa mara kwa msimu huu, hivyo siamini kama taarifa za kutaka kuondoka kwake amezitoa yeye mwenyewe katika vyombo vya habari,”

“Tulipocheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tottenham, hakuwa katika mazingira mazuri ya kucheza, jambo ambalo lilinilazimu kuwatumia wachezaji wengine waliopo kikosini ambao walikua katika hali nzuri ya kupambana.

“Kwa ujumla ninafurahishwa na Sturridge kuwepo Liverpool. Na ninawahakikishia atacheza na atafunga mabao mengi kwa msimu huu. Alisema Klopp alipozungumza na waandishi wa habari.

Amtumia mpenzi wake zawadi ya chatu akiwa hai akizuga ni ‘msosi’
Video: Majaliwa awakaribisha wawekezaji wa sekta binafsi kutoka Japan