Bosi wa kikosi cha Liverpool  Jurgen Klopp, yu tayari kumsajili mlinda mlango mashuhuri wa England Joe Hart, ambaye anaitumikia klabu ya Torino ya Italia kwa mkopo .

Hart alipelekwa kwa mkopo mjini Torino mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kiwango chake kushindwa kumridhisha meneja mpya wa klabu ya Man City Pep Guardiola.

Gazeti la The Mirror limeeleza kuwa, Klopp ana nia ya dhati ya kumsajili mlinda mlango huyo na kumpa jukumu la kuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Liverpool.

Matarajio ya meneja huyo kutoka nchini Ujerumani yamekuja kufuatia ushindani hahifu uliopo katika nafasi ya walinda milango klabuni hapo, ambapo kwa sasa kumekua hakuna uwiyano sawa kati ya Simon Mignolet na Loris Karius ambaye alimsajili akitokea Mainz.

Klopp anaamini endapo atafanikiwa kumsajili Hart, ushindani wa kweli utapatikana katika nafasi ya ulinzi wa lango na kukifanya kikosi chake kuwa na uhakika wa kipa bora.

Aliyekufa muda mfupi baada ya kubatizwa azikwa kiislam
Shahidi wa pili atoa ushahidi kumbana Lissu, akumbana na swali la Kibatala