Klabu ya Liverpool inakaribia kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya SSC Napoli ya Italia Gonzalo Higuain.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la The Sun la nchini England mapema hii leo, zinaeleza kwamba mshambuliaji huyo yu njiani kuachana na klabu yake ya SSC Napoli kwa shinikizo la kutaka kufanya kazi na meneja kutoka Ujerumani Jurgen Klopp.

Higuain ambaye alifunga mabao 36 katika michezo 35 ya ligi ya nchini Italia Sirie A msimu uliopita, amekua akiutaka uongozi wa SSC Napoli kumuachia kuondoka katika kipindi hiki, kwa kusudio la kwenda kusaka changamoto mpya katika ligi ya England.

Awali mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alikua akihusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea, kufuatia meneja mpya wa The Blues Antonio Conte kuvutiwa na uwezo wake, lakini siku chache baadae mambo yalibadilika na klabu ya Liverpool ikaanza kutajwa.

Klopp ameweka mkakati wa kufanya usajili wa mshambuliaji, kufuatia kuidhinisha mpango wa kuuzwa kwa Christian Benteke pamoja na Daniel Sturridge huku akionyesha kutaka kubaki na Roberto Firmino na Divock Origi ambao watasaidiana na mchezaji atakaemsajili.

Hector Herrera

Katika hatua nyingine Liverpool, wameripotiwa kufikia makubaliano na uongozi wa FC Porto, kwa ajili ya usajili wa kiungo kutoka nchini Mexico, Hector Herrera.

BMT Waukataa Mchakato Wa Uchaguzi Wa Young Africans
Video: Walichozungumza CCM Baada ya Upinzani Kuilalamikia Serikali Kwa Wananchi