Menaja wa majogoo wa jiji Liverpool, Jurgen Klopp muda mchache uliopita amesaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo ilimuajiri mwaka 2015, baada ya kuondoka kwa Brendan Rodgers.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports kimeripoti kwamba, bosi huyo kutoka nchini Ujerumani amekubali kusaini mkataba mpya ambao utamuweka Anfield hadi mwaka 2022.

Taarifa za kituo hicho zimeendelea kubainisha kwamba, mafanikio yaliyopatikana tangu alipoajiriwa Klopp, yamewapa mvuto viongozi wa klabu ya Liverpool na kuamini wamefanya chaguo sahihi.

Klopp aliiongoza Liverpool katika michuano ya Europa League pamoja na Capital One Cup hadi kwenye hatua ya fainali, lakini kwa bahati mbaya alipoteza michezo yote miwili ambayo ilikua muhimu kwa klabu hiyo.

Alipowasili klabuni hapo, Klopp alikua anapambwa na mafanikio aliyoyapata akiwa na klabu ya Borussia Dortmund ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ujerumani mara mbili mfululizo pamoja na kuifikisha katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mkataba wa awalia mba oKlopp aliusaini wakati akiajiriwa Liverpool mwezi Oktoba mwaka 2015, ulikua unafikia tamati mwaka 2018.

Wakati huo huo wasaidizi wake Klopp Zeljko Buvac na Peter Krawietz nao wamesaini mikataba mipya.

Video: Mwanamke aliyekolewa akiwa hai baada ya kusombwa na mafuriko kilomita 60
Video: Mambo 6 yanayomhusu Cristiano Ronaldo