Uongozi  wa klabu ya Simba umemtaka kiungo Mzimbabwe Justice Majabvi kuamua moja kama

kuendelea kuitumikia timu yao au kuondoka,Hayo yamekuja baada ya Majabvi kukataa kukaa kwenye nyumba alizooneshwa na uongozi wa klabu hiyo na kutaka atafutiwe nyumba atakayokaa na familia nzima.

Akitoa msimamo wa klabu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kama kiungo huyo atashindwa kukubaliana nao afunge safari na kuiacha klabu hiyo,Hans Poppe alisema katika mkataba waliokuwa wameingia na mchezaji huyo ulionesha kuwa watampatia malazi, lakini kila nyumba wanayomuonesha anaikataa.

Alisema mpaka sasa wameshamuonesha sehemu tatu zote anazikataa na kwa kipindi chote hicho amekuwa akiishi kwenye Hoteli ya Lamada akilipiwa kwa siku sh. 40,000.

“Huyu mchezaji hatuelewi anataka nini hasa, kwani tumeshamtafutia nyumba takribani tatu lakini zote anazikataa anataka nyumba ya peke yake na fikiria kwa sasa tunamlipia sh. 40,000 kwa siku,”alisema Hans Pope.

Alisema kwa kitendo hicho si cha kiungwana hasa kwa mchezaji wa kimataifa kama yeye kufanya vitu vya ajabu, ikiwemo kwenda kwenye vyombo vya habari kulalamika bila idhini ya uongozi,Kutokana na hilo uongozi wa Simba umemtaka Majabvi kuondoka kama anaona hajaridhishwa na mazingira ya hapa kwani wana wachezaji wengi sana nchini.

Aidha, Hans Pope alisema anashangaa sana kumsikia mchezaji huyo akisema maisha anayoishi Simba ni tofauti na timu nyingine alizochezea na hajaridhika nayo,Aliongezea kwa kusema, aende zake kwani hawatakubali kuendelea kuwa na mchezaji asiyeheshimu mkataba wake na kwenda kuwadhalilisha kwenye vyombo vya habari.

Wanyarwanda Waidhinisha Uwezekano wa Kagame Kutawala hadi 2034
Arsene Wenger Adhihirisha Kura Yake Kwa Lionel Messi