Justin Bieber ameamua kujitoa mhanga kufikisha ujumbe wenye mtazamo hasi dhidi ya mashairi ya baadhi ya nyimbo za mkongwe asiyechuja kwenye hip-hop, Eminem.

Mwimbaji huyo ametumia ukurasa wa Instagram Stories alipokuwa anasikiliza wimbo wa Eminem ‘The Ringer’ ambao uko kwenye albam yake ya ‘Kamikaze’.

Ingawa alieleza kukuubali mtindo wa michano wa rapa huyo, Bieber alieleza kuwa hakubaliani na jinsi ambavyo anawashambulia marapa wapya akieleza kuwa hafahamu muelekeo wa mawimbi ya hip-hop.

“Ninapenda mtindo wa michano wa Eminem lakini sipendi anavyowashambulia marapa wapya. Ninapenda kizazi kipya cha rap, Em hakiielewi tu,” aliongeza.

Kwenye ngoma hiyo ya ‘The Ringer’, Eminem amemchana Lil Yachty na mitindo yao mipya aliyoiita ‘mumble rap’. Lakini amewasifia wasanii kama J.Cole, Big Sean na Kendrick Lamar.

Kamikaze ni albam ya Eminem aliyoiachia Agosti 31, 2018 ikiwa na nyimbo kadhaa zilizowakwaruza wasanii wengi waliokuwa na tatizo na rapa huyo ikiwa ni pamoja na Mashine Gun Kelly na Joe Burden.

Katibu wa Uenezi CCM Njombe acharuka, ' Msiitegemee Serikali'
Habari Picha: Dkt. Raphael Chegeni azungumza na Watanzania waishio Uingereza

Comments

comments