‘Kibongobongo’, wapo waimbaji wakali kama Ali Kiba, H-Baba, Hussein Machozi ambao ukiwaweka ndani ya chaki ni kama mzimu wa Mbwana Samatta, ila ughaibuni, Justin Bieber ameamua kujinoa uso kwa uso na Neymar wa Barcelona.

bieber-na-neymar

Bieber ambaye ni shabiki mkubwa wa mpira wa miguu pamoja na masumbwi, leo alitinga katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Barcelona vya Joan Gamper na kukutana na miba mitatu ya timu hiyo, Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez.

Vyombo vya habari vya Barcelona vilivyoshuhudia tukio hilo vimeeleza kuwa baada ya kujiachia na wakali hao, Bieber aliingia uwanjani kupiga mazoezi na Neymar na Rafinha (Rafael Alcántara do Nascimento).

Neymar na Bieber walipost picha za tukio hilo mitandaoni. Huenda Bieber aliwapa faraja kufuatia kushindwa kupachika mabao katika mchezo wao wa juzi dhidi ya Malaga.

Jack Wilshere Akata Tamaa, Adhamiria Kuondoka Jumla
The Game ‘apigwa rungu’ kwa unyanyasaji wa kingono