Justin Bieber ametangaza kusitisha kufanya muziki akieleza kuwa anataka kuvuta pumzi ili atatue matatizo yanayomsibu ya kiafya na familia.

Mkali huyo wa pop ameandika kwenye Instagram akiwajibu mashabiki wake waliokuwa wakimuuliza kuhusu ujio wa albam yake mpya kwani ni muda mrefu hawajapata kitu kizito kutoka kwake.

“Kwahiyo nimesoma jumbe zenu mnasema mnataka albam mpya. Nimefanya ziara nyingi kwenye maisha yote ya utoto (hadi nikiwa na miaka 19), na hata nilipofika miaka ya 20, na nimebaini na hata nyie mliona sikuwa na furaha kwenye ziara yangu ya mwisho na sistahili hicho na nyie pia hamsitahili, mmelipa pesa ili mje muone tamasha la mtu mwenye  nguvu na sikuweza kufanya hivyo kiakili hasa mwishoni mwa ziara yangu,” tafsiri ya ujumbe wa Bieber.

Ingawa muziki bado ndio kipaumbele cha kazi zake, familia yake na afya yake ni muhimu zaidi.

“Muziki ni muhimu sana kwangu lakini hakuna kinachozidi familia yangu na afya yangu. Nitarudi na albam kali mapema iwezekanavyo,” anaeleza katika sehemu ya ujumbe huo.

Bieber ameeleza kuwa anaamini yeye atabaki kuwa juu iwe anafanya muziki au amesimama kufanya muziki.

Mwezi uliopita, E! waliripoti kuwa Justine Bieber alikuwa akikabiliwa na sonona (depression) na kwamba alikuwa katika wakati mgumu akitafuta msaada.

Mahakama ya Rufaa yapendekeza umri wa kufanya ngono kuwa miaka 16
McGregor ashtua wadau wa ngumi, atangaza kustaafu ghafla

Comments

comments