Staa Justin Beiber, ambaye hivi karibuni amefanya remix ya wimbo wa Despacito ulioimbwa na staa Luis Fonsi amepondwa vikali baada ya kushindwa kuimba kwa Lugha ya Spanish kwenye remix ya wimbo huo Despacito.

Mashabiki wa rekodi hio waliohudhuria baadhi ya show za Justin na kumuomba aimbe wimbo huo wamesema Justin amemkosea heshima Luis Fonsi kwa kufanya remix ya wimbo wake na kushindwa kuimba kwa lugha yao ya Spanish.

Kwa upande mwingine mwenye wimbo huo staa Luis Fonsi kutoka Puerto Rico amemtetea Justin Bieber nakusema staa huyu hajui lugha hio hivyo sio rahisi kushika mistari iliyopo kwenye wimbo huo kama ambavyo mashabiki walidhani.

Kwa sasa Luis Fonsi anatamba narekodi yake ya Despacito aliyomshirikisha Daddy Yankee.

Tazama video remix ya Justin Beiber akiimba wimbo wa Despacito.

Ng'ombe 165 wasafirishwa kwa ndege kwenda Qatar
Wananchi 121 wa Uganda watoweka