Beki wa Simba, Juuko Murshid ametua mjini Mbeya tayari kuwavaa wenyeji Mbeya City, kesho.

Simba tayari ipo mjini Mbeya lakini Juuko alikuwa na majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Uganda iliyokuwa inaivaa Ghana katika mchezo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018.

“Kweli Juuko ameshatua na ameungana na wenzake na leo tutafanya naye mazoezi mepesi,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.

Simba imekuwa ikiendelea na maandalizi yake vizuri kujiandaa kuivaa Mbeya City ambayo inaonekana kuupania mchezo huo.

Wijnaldum Amuweka Njia Panda Jurgen Klopp
Hans van der Pluijm Apangua Taarifa Za Kutimuliwa